5 Juni 2025 - 16:50
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Haki za Nyuklia za Iran Lazima Ziheshimiwe Katika Mazungumzo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Uhuru wa Kisiasa ni Asili ya Sera ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu – Haki za Nyuklia Lazima Zihifadhiwe Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo maalum amesisitiza kuwa uhuru wa kisiasa ni nguzo kuu ya sera ya kigeni ya Iran, akieleza kuwa taifa hilo limekuwa likijitahidi daima kujiepusha na utegemezi au kuingiliwa na madola ya kigeni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Kuhusu suala la kumiliki teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani na urutubishaji wa urani, Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa jambo hili linatokana na mahitaji halisi ya jamii ya Iran.

Ameongeza kwa kusema:
"Kanuni muhimu zaidi katika sera ya kigeni ya Iran ni suala la uhuru na kujitegemea."

Akaeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imeweka msimamo thabiti wa kujiepusha na utegemezi wa kisiasa kwa madola ya nje, na kwamba sera ya nyuklia ya nchi hiyo inaendeshwa kwa misingi ya haki, uhalali wa kisheria, na mahitaji ya maendeleo ya taifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Kiongozi Mkuu wa Masuala ya Kisheria na Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kazem Gharibabadi, amesema:

Katika mahojiano na tovuti ya Khamenei.ir, yaliyofanyika pembeni mwa kumbukumbu ya kifo cha Imam Khomeini (r.a), Gharibabadi alieleza kuwa misingi ya sera ya kigeni ya Iran imejengwa juu ya Katiba ya nchi na mafundisho ya Imam Khomeini.

Akasema:“Kanuni kuu katika sera ya kigeni ya Iran ni uhuru wa kisiasa, unaotokana na kanuni ya ‘Nafy Sabil’ (kutokubali udhibiti wa wageni).”

Akaongeza kuwa tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, serikali zote za Iran zimepanga sera zao za kigeni kwa msingi wa uhuru, na bado mpaka leo nchi inaendelea kwa msingi huo.“Sera zetu za kigeni zimejikita kwenye maslahi ya taifa, usalama wa kitaifa, na manufaa ya wananchi wetu, si kwa matakwa ya mataifa yenye nguvu,” alisisitiza.

Gharibabadi pia alisema kuwa:“Katika dunia ya leo, nchi nyingi ziko chini ya ushawishi wa mataifa makubwa katika sera zao za nje, lakini Iran imekuwa ikijitahidi kujiepusha na utegemezi huo.”

Kuhusu Mazungumzo ya Nyuklia:

Gharibabadi alisema kuwa katika mazungumzo ya kimataifa, suala muhimu kwa Iran daima limekuwa ni kutambuliwa na kuheshimiwa kwa haki ya Iran ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani.“Tumewekeza raslimali kubwa katika teknolojia ya nyuklia na pia tumetoa mashujaa wetu – mashahidi wa nyuklia – katika njia hii. Hivyo basi, teknolojia hii ni haki yetu ya kimsingi na inatokana na mahitaji halisi ya jamii ya Iran.”

Akaeleza kuwa teknolojia ya kurutubisha urani ni ya kisasa na ni wachache tu duniani wanaomiliki mzunguko kamili wa nishati ya nyuklia – na Iran ni miongoni mwao.“Sababu ya vikwazo dhidi yetu ni kwa sababu tumeingia kwenye uwanja ambao ni mstari mwekundu kwa mataifa machache yenye nguvu.”

Katika hitimisho lake, Gharibabadi alisema:“Katika kila mchakato wa mazungumzo, haki hii ya taifa la Iran ni kipaumbele, na haitakiwi kuathiriwa kwa namna yoyote.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha